Kompyuta
ni nini?
Umeanza
kutumia kompyuta?, je una maswali unaposikia watu wanasema maneno na misamiati
ya kompyuta na ukashindwa kuelewa?, bas makala hii itajadili mada yenye
kutambulisha kwako mambo muhimu yanayohusu kompyuta. Usiwe na hofu, kwa sababu
tulipofikia kwa sasa hatuwezi kukwepa kutumia kompyuta, hivyo ukiwa na uelewa
kidogo tu utakaojifunza hapa, utafahamu kompyuta ni nini na utabaini aina mbali
mbali za kompyuta zilizopo. haya tuanze kujifunza. Kompyuta ni nini?
Kompyuta ni kifaa cha ki elektroniki ambacho hufanya kazi kwa
kuendesha taarifa, au data.
Kifaa hichi kina uwezo wa kuhifadhi, kuchambua,
na kuchakata data/taarifa. Bila shaka unafahamu
kuwa waweza tumia kompyuta kuchapa nyaraka mbalimbali, kutuma
barua pepe, kucheza michezo, na kuvinjari
mtandaoni. Waweza pia kutumia kompyuta kuhariri
picha, video na mambo mengine mengi. Tafadhali
angalia picha hii hapa chini kuona watu mbali mbali wakitumia kompyuta (Picha
hii nimeitoa mtandaoni kwanuani hii).
Vifaa na Programu za
Kompyuta.
Kabla hatujajifunza
aina za kompyuta, tujifunze vitu/mambo muhimu yanayokamilisha kompyuta.
Kumpyuta ina sehemu kuu mbili, Vifaa ( Hardware ) na Programu (Software).
Vifaa(Hardware)
vinashikika na ndio vinaunda mifumo ya ki elekroniki ambayo inaonekana
kifizikia mfano, kipanya(mouse), kiambaa (keyboard), Kioo cha kuangalizia
(Monitor/screen) na vyote vilivyomo ndani ya kasha la kompyuta.
Programu(Software)
hazishikiki, ni mkinyaiko wa maelekezo ya kuviongoza vifaa vifanye kazi na
kusababish amatokeo ambyo mtumiaji anataka yatokee kwenye kila jambo. Mfano wa
programu ni kivinjari cha wavuti (web browser) au programu ya kuandika
nyaraka ya Microsoft Word, na zingine nyingi ambazo tutajifunza huko mbele.
Kimsingi hizi programuu ndizo zinazofanya watu wafurahie na wanufaike kutumia
kompyuta lakini zitafanya yote juu ya vifaa vyenye uwezo wa kupokea maelekezo
hayo.
Chochote unachofanya
kwenye kompyuta hutegema vifaa na programu. Mfano hivi sasa yawezekana unasoma
makala hii kwa kutumia kivinjari (web browser) ikiwa ndani ya kompyuta ya
mezani, na unatumia kipanya(mouse) kubofya viungo vilivyomo kwenye kurasa ili
kufungua kurasa zingine kwenye tovuti hui au nyinginezo. Na baada ya kujifunza
aina za kumpyuta utajiuliza kwenye aina tofauti za kompyuta hizo ni vifaa gani
vinaweza kutumika kama kipanya.
Aina za kompyuta
Wengi wanaposikia
kompyuta huelekeza mawazo yao kwenye kompyuta za mezani (Desktop Computers) au
kompyuta za mpakato (Laptop Computers), lakini ukweli ni kwamba kuna aina
nyingi za kompyuta zaidi ya hizo mbili nilizokwisha zitaja hapa. Na kwa
maendeleo ya tekinolojia yalipofikia hivi sasa, ni muhimu ukafahamu kuwa kompyuta
zimetuzunguka kila mahali, ziko mezani, mikononi, barabarani, hospitali, na
kila mahali.
Kimsingi kompyuta
zimegawanyika katika makundi makuu mawili, kuna kompyuta za madhumuni
ya jumla (General purpose computers) hizi ndio wengi wanazitambua na
kuzibainisha moja kwa moja kama kompyuta, lakini pia ziko kompyuta za
kusudi maalumu (Special purpose computers) mfano, kikokotozi (calculator)
ni kompyuta kwa ajili ya kukokotoa tu. Vifaa vingi vya eletroniki mfano luninga
(TV), Saa za digitali (digital watches), kisimbuzi (decoders), simu za mkononi
za kawaida (feature phones) zina kompyuta maalumu kwa kazi yake, na zina uwezo
wa kuhifadhi, kuchakata, na kuendesha data kulingana na mipaka yake.
Tujifunze sasa baadhi
ya kompyuta ambazo wengi huzibainisha moja kwa moja, mada yakuelekeza aina zote
za kumpyuta na zinavyofanya kazi iko inje ya makala hii, badala yake
tutaangazia zaidi kompyuta zinazotumiwa na watu binafsi zaidi (personal
computers), kama zifuatavyo.
Kompyuta ya mezani
(Desktop Computer)
Hizi utazikuta sana
maofisini, majumbani, mashuleni nakadhalika, zinakaa juu ya meza, zaweza kuwa
ndogo, saizi ya kati, au kubwa sana kimuonekano lakini umbile sio lazima
lishabihiane na uwezo, tutakuja kujifunza sifa zinazoipa uwezo kompyuta kwenye
makala nyingine. Mara nyingi iko pembeni ya Kioo cha kungalizia (monitor) , pia
imeunganishwa na kipanya (mouse), na kiambaa (keyboard).

Konpyuta ya mezani ni
rahisi kuiboresha kwa kuongezea vitu, na pia bei yake ni rahisi kwa sababu
vifaa vyake hutengezwa kwa maumbile makubwa kiasi ambvyo kitekinolojia sio
ghali kuvitengeneza ukilinganisha na vifaa vya kompyuta ndogo kiumbo.
Uliknganisha kumpyuta ya mezani na ya mpakato zenye uwezo sawa, utakuta ya
mezani ni ya gharama nafuu sana kwa bei.
Kompyuta ya kupakata
(Laptop computer)
Hii ni aina ya pili
maarufu ya kompyuta binafsi, ni ndogo na zinabebekam hivyo waweza kuzitumia
karibu kila mahali uendapo kwa sababu zinatumia betri ya kuchaji. Mara zinatuza
chaji kwa muda zaidi ya masaa mawili, hivyo wengi wanafurahia kuzitumia kwa uhuru
wa kuweza kutembea nazo.

Kutokana na udogo wake
sio rahisi sana kuziongezea au kubadilisha vifaa vyake vya ndani kama ambvyo
ungefanya kwenye kompyuta za mezani, inagawa inawezekana, alini huwa
zimetengezwa na sifa zenye kuifaa ikiwa hivyo, labda itokee kifaa kimeharibika.
Kipanya na kiambaa ni
sehemu ya kompyuta hii, ila pia waweza kuunga vifaa vya pembeni endapo
utahitaji.
Kompyuta Kibao (Tablet
computer)
Kompyuta kibao ni
kompyuta ndogo zaidi ya kompyuta mpakato, yenyewe ni ya kushika mhononi tu, na
rahisi zaidi kutembea nayo popote, na huwa zikikaa na chaji kuliko za kupakata.
Badala yakutumia kipanya na kiambaa, yenyewe unagusa na vidole vyako kwenye
kioo ili kuandika au kuperuzi, pia zingine huwa na kalamu maalumu (Stylus)
unayoweza kuchora au kuandika juu ya kioo chake. iPad ni mfano wa kompyuta
maaarufu ya namna hii.

Kompyuta hizi,
hafinayi kila kitu ambacho ya mezani au ya kupakata yaweza fanya, lakini waweza
kuitumia kama unataka kujisomea, kucheza michezo, kuwasiliana na watu kwenye
mitandao ya kijamii, kusoma barua pepe, na kujiburudisha kwa kusikiliza miziki
na kuangalia video. Kutokana na muundo na malengo ya matumizi yake, hazina
uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kuchakata data, na utaifurahia zaidi kama utakuwa
na mtandao wa wavuti(internet), kwa mtu mwenye kuihitaji burudani na kupata
taarifa kwa urahisi popote alipo, kompyuta hizi huwafaa sana, lakini bado
utahitaji kuwa na ya mezani au ya kupakata ili uweze kufanya kazi zingine za
kompyuta kama kuchapa nyaraka n.k.
Seva kompyuta (Server)
Seva ni kompyuta
ambayo inahudumia kompyuta zingine zilizo kwenye mtandao, mtandao unaweza kuwa
wa ndani ya ofisi (local area network), au mtandao wa wavuti (internet).
Makampuni mengi yanatumia seva kuifadhi mafaili na kutoa huduma zigine kwa
wafanyakazi na pia kitoa taarifa kwa wateja mbalimbali. Seva yaweza kuonekana
kama kama kompyuta ya kawaida au yenye umbile kubwa zaidi, na kwenye makampuni
makubwa seva hutengawa kwenye vyumba maalumu na hutunzwa kwa mumakini mkubwa
kwa sababu zintegemewa na mamilioni ya wahiyajio huduma.

Seva ndio mchezaji
mkuu wa mtandao, ndio wanaofanya watu kuwa na tovuti duniani, na ndio
vichochezi vya tekinolojia ya wingu la makompyuta (cloud computing).
Unapoangalia muziki kwenye tovuti ya
www.youtube.com video
zote hizo zimehifadhiwa kwenye seva, na seva inakuhudumia video unayotaka
kuiona kwenye kompyuta yako, ba inafanya hivyo kwa ziadi ya kompyuta milioni
kwa wakati mmoja, hivyo seva zina uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi na kuchakata
data, na ni gharama kuziunda, na kuzitunza pia.
Aina nyigine za
kompyuta
Kama nilivyogusia
awali, leo hii kuna aina lukuki za kompyuta ambazo kwa kiasi kikubwa ni za
matumizi maalumu. Ili kuongezea elimu yetu hii, nitaorodhesha baadhi ya
kompyuta hizo:-
1.
Simu
za mikononi – wengi
wanatumia simu za mikononi za kisasa (Smartphones) kufanya mambo mengi amabyo
ungeweza kufanya kwenye kompyuta ya mezani kama kucheza michezo (games), kusom
abarua pepe, na kuangalia mztandao pia kuwasiliana na marafiki kwenye mitandao
ya kijamii
2.
Kumpyuta
za michezo (Game consoles) –
mfano playstation, nintendo n.k, hizi ni kompyuta maalumu kwa michezo ya kwenye
luninga, mfano mpira, magari n.k.
3.
Luninga
(TV) – hizi za kisasa
zinauwezo wa kuunganisha kwenye mtandao wa wavuti na kufungua taarifa mbali
mbali
Hitimisho
Tumejifunza kompyuta
ni nini?, na watu hutumia kompyuta kufanya mambo gani, pia tumeona baadhi ya
aina mbali mabli za kompyuta na kufahamu matumizi yake na mipaka yake kwa
ujumla. Somo hili halitaishia hapa kwani bado kuna mengi ya kujifunza kuhusu
kompyuta hizi, kwenye makala nyingine tutajifunza kuhusu uwezo wa kumpyuta na
unaweza vipi kufahamu, pia sifa za programu endeshi za kompyuta hizo.
Tafadhali anedela
kufungua tovuti hii ili uweze kujifunza zaidi kuhusu mambo ya TEHAMA http://benloti.com/2016/04/12/kompyuta
0 maoni:
Chapisha Maoni
Jinsia
Umri
Unaishi wapi